Mistari ya Biblia Kuhusu Imani Huhamisha Milima
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Imani Huhamisha Milima ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Aliwaambia, “Ni kwa sababu imani yenu ni ndogo mno. Kweli nawaambia, kama mna imani hata iliyo ndogo kama mbegu ya haradali, mnaweza kuuambia mlima huu, ‘Toka hapa uende pale,’ nao utakwenda. Hakuna jambo ambalo hamtaweza kulifanya.”
Kweli nawaambia, mtu akiuambia mlima huu, ‘Ondoka, ukatupwe baharini,’ bila kusitasita moyoni mwake, bali akiamini kwamba anachokisema kinatokea, atafanyiwa hivyo.
Yesu akawajibu, “Kweli nawaambia, mkiwa na imani na msipokuwa na shaka, mtafanya zaidi ya lile lililofanyika kwa mtini huu. Hata mkiuambia mlima huu, ‘Uinuliwe na kutupwa baharini,’ itafanyika.
Yesu akamwambia, “’Kama unaweza!’ Kila kitu kinawezekana kwa mtu anayeamini.”
Bwana alijibu, “Kama mngekuwa na imani yenye ukubwa wa mbegu ya haradali, mngeweza kuuambia mforsadi huu, ‘Jing’oe na mizizi yako, ukajipande baharini,’ nao ungefanya mnavyosema.
Na chochote mtakachoomba katika maombi mtakipokea, ilimradi mnaamini.”
Kwa hiyo nawaambia: chochote mnachoomba mnaposali, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtakipata.
Huenda nikaweza kutoa unabii, na kuelewa kila siri na kila kitu kinachoweza kujulikana; huenda nikawa na imani yote iliyopo, ya kutosha kuhamisha milima; lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu.
Kisha akayagusa macho yao, akasema, “Kwa sababu ya imani yenu, na iwe hivyo kwenu.”
Ninazo nguvu za kukabili kila hali ndani ya yule anayenifanya kuwa na nguvu.
Kupitia imani walishinda falme, walitawala kwa haki, walipata yale yaliyoahidiwa, na walifunga vinywa vya simba.
Lakini aombe kwa imani, bila kusitasita. Mtu anayesitasita ni kama wimbi la bahari kuu, linalosukumwa na upepo na kutupwa huku na huku.