Mistari ya Biblia Kuhusu Mpatanishi

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Mpatanishi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Timotheo 2:5

Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu,

02 Waebrania 9:15

Kwa sababu hii Kristo ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.

03 Waebrania 12:24

kwa Yesu mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Abeli.

04 1 Yohana 2:1

Watoto wangu wapendwa, nawaandikia haya ili msitende dhambi. Lakini kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba: ndiye Yesu Kristo, Mwenye Haki.

05 Wagalatia 3:20

Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja.

06 Waebrania 8:6

Lakini huduma aliyopewa Yesu ni bora zaidi kuliko yao, kama vile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani, nalo limewekwa misingi wa ahadi zilizo bora zaidi.

Mada zinazohusiana