Mistari ya Biblia Kuhusu Mchungaji Mkuu

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Mchungaji Mkuu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Waebrania 13:20

Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo,

02 1 Petro 5:4

Naye Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea taji ya utukufu isiyoharibika.

03 1 Petro 2:25

Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmerudi kwa Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.

04 Yohana 10:11

“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.

05 Zaburi 23:1

Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.

06 Yohana 10:14

“Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu nao kondoo wangu wananijua.

07 Isaya 40:11

Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo: Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake na kuwachukua karibu na moyo wake, huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.

08 Ezekieli 34:23

Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao.

Mada zinazohusiana