Mistari ya Biblia Kuhusu Ameketi Mkono wa Kuume wa Mungu
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Ameketi Mkono wa Kuume wa Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
ambazo alizitumia katika Kristo alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha upande wake wa kulia katika ulimwengu wa mbinguni,
Mwana ni mwangaza wa utukufu wa Mungu na mfano kamili wa kiini chake, naye anavitegemeza vitu vyote kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kufanya usafishaji wa dhambi kupitia nafsi yake, aliketi upande wa kulia wa Ukuu aliye juu.
Mmefufuliwa pamoja na Kristo; kwa hiyo tafuteni yale yaliyo juu, mahali ambapo Kristo ameketi upande wa kulia wa Mungu.
Kwa hiyo Bwana Yesu, alipokwisha kuzungumza nao, alipandishwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
Ya Daudi. Zaburi. BWANA amwambia bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, nami niwaweke adui zako chini ya miguu yako kama kiti cha kuwekea miguu.”
Lakini kuhani huyu alitoa dhabihu moja tu kwa ajili ya dhambi, inayofaa kwa wakati wote, kisha akaketi upande wa kulia wa Mungu.
Je, Mungu amewahi kumwambia malaika yeyote, “Keti upande wa kulia wangu, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako kama kigoda”?
Kwa hiyo sasa ameinuliwa hadi upande wa kulia wa Mungu. Alipokea kutoka kwa Baba Roho Mtakatifu aliyeahidiwa, na sasa amemimina hiki mnachokiona na kukisikia.