Mistari ya Biblia Kuhusu Kupima Kila Kitu

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kupima Kila Kitu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema.

02 1 Yohana 4:1

Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.

03 Matendo 17:11

Hawa Waberoya walikuwa waungwana zaidi kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.

04 Warumi 12:2

Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.

05 Wafilipi 1:9-10

Haya ndiyo maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo,

06 1 Wakorintho 14:29

Manabii wawili au watatu wanene na wengine wapime yale yasemwayo.

Mada zinazohusiana