Mistari ya Biblia Kuhusu Habari Njema kwa Maskini

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Habari Njema kwa Maskini ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Luka 4:18

“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa,

02 Isaya 61:1

Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu Bwana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao;

03 Mathayo 11:5

Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.

04 Luka 6:20

Akawatazama wanafunzi wake, akasema: “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu.

05 Yakobo 2:5

Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?

06 Zaburi 34:6

Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

07 Isaya 61:1-2

Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu Bwana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao; kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi ya Mungu wetu, kuwafariji wote waombolezao,

08 Zaburi 9:18

Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.

09 Luka 1:53

Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.

10 Zaburi 113:7

Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,

11 1 Samweli 2:8

Humwinua maskini kutoka mavumbini na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu; huwaketisha pamoja na wakuu na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima. “Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Bwana; juu yake ameuweka ulimwengu.

Mada zinazohusiana