Mistari ya Biblia Kuhusu Neema na Matendo
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Neema na Matendo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Halitokani na yale ambayo mtu yeyote ametenda, kwa hiyo hakuna nafasi ya mtu yeyote kujisifu.
Kwa maana ni kwa neema hiyo mmeokolewa, kupitia imani. Jambo hili halitoki kwenu; ni zawadi ya Mungu. Halitokani na yale ambayo mtu yeyote ametenda, kwa hiyo hakuna nafasi ya mtu yeyote kujisifu.
Hata hivyo tunajua kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria; mtu huhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Yesu Kristo tu. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Kristo Yesu, ili tuhesabiwe haki kwa imani katika Kristo wala si kwa matendo ya sheria, kwa sababu hakuna binadamu atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria.
Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, ila anamwamini Mungu anayemhesabia haki mtu asiyemcha Mungu, imani hiyo inahesabiwa kuwa haki.
alituokoa, si kwa sababu ya mambo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kupitia kuoshwa kunakoleta kuzaliwa upya na kufanywa wapya na Roho Mtakatifu,
Kwa njia ya sheria hakuna mtu anayehesabiwa haki machoni pa Mungu; hilo ni wazi, kwa kuwa “Mtu aliye mwenye haki ataishi kwa imani.”
Mshahara wa mfanyakazi hauhesabiwi kuwa neema, bali kuwa deni analostahili kulipwa.
Na ikiwa ni kwa neema, basi haitokani tena na matendo; vinginevyo neema ingekoma kuwa neema.
na nionekane kuwa ndani yake, bila haki yangu mwenyewe inayotokana na kuishika sheria, bali nikiwa na haki inayopatikana kupitia imani katika Kristo: haki itokayo kwa Mungu, inayotegemea imani.