Mistari ya Biblia Kuhusu Jipatie Hekima
Mistari 7 ya Biblia kuhusu Jipatie Hekima ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.
Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha!
kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.
Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu.
Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako, kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu, na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu, na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa, ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu.
Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.