Mistari ya Biblia Kuhusu Kukata Tamaa

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Kukata Tamaa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 42:11

Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa sababu bado nitamsifu, Mwokozi wangu na Mungu wangu.

02 2 Wakorintho 4:8-9

Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.

03 Zaburi 34:18

Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.

04 Maombolezo 3:21-23

Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.

05 Zaburi 40:1-2

Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu. Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama.

06 Zaburi 27:13-14

Nami bado nina tumaini hili: nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai. Mngojee Bwana, uwe hodari na mwenye moyo mkuu, nawe, umngojee Bwana.

07 Warumi 8:38-39

Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu, Bwana wetu.

08 Zaburi 73:26

Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.

09 Mika 7:8

Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu! Ingawa nimeanguka, nitainuka. Japo ninaketi gizani, Bwana atakuwa nuru yangu.

Mada zinazohusiana