Mistari ya Biblia Kuhusu Tumaini Lililo Hai

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Tumaini Lililo Hai ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 9 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 1 Petro 1:3 Mstari mkuu

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema yake kuu ametupa kuzaliwa upya. Kupitia kufufuka kwa Yesu Kristo kutoka kwa wafu ametuleta katika tumaini lenye uzima,

02 Warumi 15:13

Mungu wa tumaini awajaze furaha na amani ya kila namna mnapoamini, ili kwa uweza wa Roho Mtakatifu mjae tumaini hadi kufurika.

03 Tito 3:5

alituokoa, si kwa sababu ya mambo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kupitia kuoshwa kunakoleta kuzaliwa upya na kufanywa wapya na Roho Mtakatifu,

04 Warumi 6:4

Basi kupitia ubatizo tulizikwa pamoja na yeye katika kifo, ili kama Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, sisi pia tuishi maisha mapya.

05 Wakolosai 1:27

Mungu aliamua kuwajulisha jinsi siri hii ilivyo na utajiri mwingi na utukufu kati ya watu wa mataifa. Siri yenyewe ni hii: Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.

06 1 Petro 1:4

na katika urithi ambao hauwezi kamwe kuoza, wala kuchafuliwa, wala kunyauka. Urithi huo unahifadhiwa salama mbinguni kwa ajili yenu,

07 Warumi 5:5

Na tumaini hili halituachi na aibu, kwa maana Mungu ametupa Roho Mtakatifu, na kupitia Roho upendo wake umejaa tele mioyoni mwetu.

08 Waebrania 6:19

Tumaini hili ni letu kama nanga ya nafsi, nanga inayoshika salama na imara, nayo hufika katika sehemu ya ndani nyuma ya pazia.

09 1 Petro 1:23

Mmezaliwa upya, si kwa mbegu inayokufa, bali kwa mbegu isiyoweza kufa, kupitia neno la Mungu, lililo hai na linalodumu.

Mada zinazohusiana

Kutoka kwa miongozo