Mistari ya Biblia Kuhusu Kufundishwa kwa Adhabu
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kufundishwa kwa Adhabu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Wakati yanapotolewa, hakuna malezi yanayoonekana kuwa jambo la furaha; yanaonekana kuwa jambo la huzuni. Lakini baadaye huwalipa wale waliofanyishwa mazoezi nayo mavuno ya amani, yaani haki.
Wale ambao Bwana anawapenda huwaadibisha, na kila mwana anayemkubali kuwa wake humcharaza mjeledi.”
Mwanangu, usiipuuze nidhamu ya BWANA, wala usichoke na maonyo yake, kwa maana BWANA humrekebisha yule ampendaye, kama baba amrekebishavyo mwana aliye furaha yake.
Badala yake, nauadhibu mwili wangu kwa mapigo na kuutendea kama mtumishi wangu, ili baada ya kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisije nikaonekana sifai.
Basi tambua moyoni mwako kwamba BWANA Mungu wako anakuadibu kama baba amwadibuvyo mwanawe.
Wote ninaowapenda ninawaonya na kuwafundisha nidhamu. Basi uwe na bidii, ukatubu.