Mistari ya Biblia Kuhusu Uanafunzi
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Uanafunzi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Basi nendeni, mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi: wabatizeni katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,
Kisha akawaambia wote, “Yeyote anayetaka kuja nyuma yangu ni lazima ajikane, aubebe msalaba wake kila siku, na aendelee kunifuata.
Kisha Yesu akawaambia Wayahudi waliokuwa wamemwamini, “Mkikaa katika neno langu, hakika ninyi ni wanafunzi wangu. Mtaijua kweli, na kweli itawafanya kuwa huru.”
Vaeni nira yangu shingoni mwenu, mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa ni mpole na moyo wangu ni mnyenyekevu. Ndipo mtakapopata pumziko kwa nafsi zenu.
Mkiwa na upendo kwa kila mmoja, kwa hili kila mtu atajua kwamba ninyi ni wanafunzi wangu.”
Mtu asipoubeba msalaba wake mwenyewe na kutembea nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Kisha Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Yeyote anayetaka kuja nyuma yangu lazima ajikane, aubebe msalaba wake, na anifuate.
Yeyote anayenitumikia lazima anifuate, na mtumishi wangu atakuwa pale nilipo. Baba atamheshimu yeyote anayenitumikia.