Mistari ya Biblia Kuhusu Ukuaji wa Kiroho
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Ukuaji wa Kiroho ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Badala yake, endeleeni kukua katika neema inayotoka kwa Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, na katika kumjua yeye. Utukufu na uwe wake, sasa na hadi siku ya milele. Amina.
Kama vichanga vilivyozaliwa karibuni, tamanini sana maziwa safi ya neno la Mungu, ili kwa hayo mkue mpaka mfikie wokovu,
ili mpate kuishi maisha yanayomstahili Bwana na kumpendeza katika kila jambo, mkizaa matunda katika kila aina ya kazi njema na kukua katika kumjua Mungu.
Badala yake, tukisema kweli kwa upendo, inatupasa kukua katika kila hali kuelekea kwake, yeye aliye kichwa, Kristo.
Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya mifereji ya maji, unaozaa matunda msimu wake unapofika, na ambao majani yake hayakauki kamwe. Lolote analolifanya linamwendea vizuri.
Nina hakika na jambo hili: aliyeanza kazi njema ndani yenu ataendelea nayo mpaka aikamilishe siku ya Kristo Yesu.
Na hili ndilo ninaloomba: kwamba upendo wenu uzidi kufurika zaidi na zaidi, pamoja na ujuzi kamili na utambuzi wa kila aina,
Kwa upande wenu, Bwana awajaze upendo hadi ufurike, upendo wa ninyi kwa ninyi na kwa watu wote, kama upendo tulio nao kwenu.