Mistari ya Biblia Kuhusu Utakaso
Mistari 7 ya Biblia kuhusu Utakaso ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu: kwamba mwe watakatifu. Jiepusheni na uasherati.
Badala yake, ninyi wenyewe muwe watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, kwa sababu imeandikwa, “Mnapaswa kuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu.”
Uwaweke wakfu kwa ajili yako kwa njia ya kweli; neno lako ni kweli.
Jitahidini kuwa na amani na kila mtu, na kuufuata utakatifu, kwa kuwa bila huo hakuna atakayemwona Bwana.
Wale wanaojitunza wakawa safi mbali na mambo hayo watakuwa vyombo vya kazi maalum, vilivyotakaswa, vyenye manufaa kwa Bwana wa nyumba, na tayari kwa kila kazi njema.
Lakini sisi imetupasa kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, ndugu mnaopendwa na Bwana, kwa sababu Mungu aliwachagua, kama malimbuko ya mavuno, ili mwokolewe kupitia Roho anayewafanya watakatifu na kupitia imani yenu katika kweli.
Sasa, hata hivyo, mkiwa huru kutoka kwa dhambi na mmefanywa watumwa wa Mungu, mna tunda linaloleta utakatifu, na matokeo yake ni uzima wa milele.