Mistari ya Biblia Kuhusu Siri ya Injili

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Siri ya Injili ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 7 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Wakolosai 1:26 Mstari mkuu

siri iliyokuwa imefichwa katika nyakati zote na vizazi vyote vilivyopita, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake.

02 Wakolosai 1:27

Mungu aliamua kuwajulisha jinsi siri hii ilivyo na utajiri mwingi na utukufu kati ya watu wa mataifa. Siri yenyewe ni hii: Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.

03 Waefeso 3:6

Siri yenyewe ni hii: kupitia Injili, watu wa mataifa ni warithi wenza, ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki pamoja ahadi iliyo katika Kristo Yesu.

04 Waefeso 1:9

Ametujulisha siri ya mapenzi yake, kama ilivyompendeza kufanya. Aliweka kusudi hili ndani ya Kristo

05 1 Timotheo 3:16

Bila shaka yoyote, siri ya imani yetu ni kubwa: Yeye alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa mwenye haki na Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa kati ya mataifa, akaaminiwa ulimwenguni kote, akachukuliwa juu katika utukufu.

06 Waefeso 3:9

na kuwaonyesha watu wote waziwazi jinsi siri hiyo inavyotekelezwa, siri ambayo kwa enzi zote zilizopita ilifichwa ndani ya Mungu, aliyeumba vitu vyote.

07 1 Wakorintho 2:7

Badala yake, hekima tunayoinena ni ya Mungu mwenyewe, siri ambayo imekuwa imefichwa. Mungu aliipanga kabla ya nyakati kwa ajili ya utukufu wetu.

Mada zinazohusiana