Mistari ya Biblia Kuhusu Nuru ya Ulimwengu

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Nuru ya Ulimwengu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 7 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Yohana 8:12 Mstari mkuu

Yesu akasema nao tena: “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Wale wanaonifuata hawatatembea gizani kamwe; watakuwa na nuru ya uzima.”

02 Yohana 1:4-5

Ndani yake kulikuwa na uzima, na uzima huo ulikuwa nuru ya watu wote. Nuru inang’aa gizani, na giza halijaishinda.

03 Yohana 9:5

Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.”

04 Yohana 12:46

Nimekuja ulimwenguni kama nuru, ili yeyote anayeniamini asikae gizani.

05 1 Yohana 1:5

Basi ujumbe tuliousikia kutoka kwake na tunaowatangazia ni huu: Mungu ni nuru, na ndani yake hamna giza hata kidogo.

06 Mathayo 5:14

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa juu ya kilima hauwezi kufichika.

07 Matendo 13:47

Kwa maana hii ndiyo amri ambayo Bwana ametupa: ‘Nimekuweka kuwa nuru kwa mataifa, ili uwe njia ya wokovu mpaka sehemu za mbali kabisa za dunia.’”

Mada zinazohusiana