Mistari ya Biblia Kuhusu Kufanyika Mwili
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Kufanyika Mwili ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Neno akawa mwili, akafanya makao yake kati yetu. Tumeuona utukufu wake, utukufu wa Mwana wa pekee aliyetoka kwa Baba, akiwa amejaa neema na kweli.
Yeye, ingawa alikuwa katika umbo la Mungu, hakuona kuwa sawa na Mungu kuwa jambo la kutumia kwa faida yake. Badala yake, alijifanya mwenyewe kuwa mtupu, akachukua umbo la mtumishi na kushiriki mfano wa wanadamu. Na alipoonekana kwa sura ya nje kama mwanadamu,
Lakini wakati ambao Mungu aliuweka ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana wake. Alizaliwa na mwanamke, akazaliwa chini ya sheria,
Basi, kwa kuwa watoto wanashiriki maisha ya pamoja ya mwili na damu, yeye mwenyewe aliyapokea maisha hayo hayo kwa namna ile ile, ili kwa kifo chake amnyang’anye nguvu yule anayeshika mamlaka ya kifo, yaani Ibilisi,
Bila shaka yoyote, siri ya imani yetu ni kubwa: Yeye alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, akathibitishwa kuwa mwenye haki na Roho, akaonekana na malaika, akahubiriwa kati ya mataifa, akaaminiwa ulimwenguni kote, akachukuliwa juu katika utukufu.
Sheria haikuwa na uwezo, kwa kuwa asili ya dhambi iliidhoofisha. Kwa hiyo Mungu alitenda. Alimtuma Mwana wake mwenyewe akiwa na mfano wa mwili wenye dhambi, kama sadaka kwa ajili ya dhambi, na katika mwili huo akaitolea dhambi hukumu.
Kwa kweli mnaijua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo: yeye aliyekuwa tajiri alifanyika maskini kwa ajili yenu, ili kwa umaskini wake ninyi mtajirike.
Hivi ndivyo mnavyomtambua Roho wa Mungu: kila roho inayomkiri Yesu Kristo kuwa amekuja katika mwili inatoka kwa Mungu,