Mistari ya Biblia Kuhusu Mkate wa Uzima

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Mkate wa Uzima ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 5 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Yohana 6:35 Mstari mkuu

Yesu akawaambia, “Mimi ni mkate wa uzima. Wanaokuja kwangu hawatakuwa na njaa kamwe, na wanaoniamini hawatakuwa na kiu wakati wowote.

02 Yohana 6:51

Mimi ni mkate ulio hai, ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakaoutoa ni mwili wangu, nami nautoa ili ulimwengu upate uzima.”

03 Yohana 6:33

Kwa maana mkate wa Mungu ni ule unaoshuka kutoka mbinguni na kutoa uzima kwa ulimwengu.”

04 Yohana 4:14

Lakini hakuna atakayekunywa maji nitakayompa atakayeona kiu tena kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ambayo maji yake yanabubujika hadi uzima wa milele.”

05 Mathayo 4:4

Lakini Yesu alijibu, “Maandiko yanasema, ‘Hakuna mtu anayeishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.’”

Mada zinazohusiana