Mistari ya Biblia Kuhusu Mwenye Haki Ataishi kwa Imani

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Mwenye Haki Ataishi kwa Imani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 6 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Warumi 1:17 Mstari mkuu

Ndani ya Injili haki ya Mungu inafunuliwa, kutoka imani kwa ajili ya imani. Kama ilivyoandikwa, “Mtu aliye mwenye haki ataishi kwa imani.”

02 Wagalatia 3:11

Kwa njia ya sheria hakuna mtu anayehesabiwa haki machoni pa Mungu; hilo ni wazi, kwa kuwa “Mtu aliye mwenye haki ataishi kwa imani.”

03 Waebrania 10:38

“Lakini mtu wangu mwenye haki ataishi kwa imani; naye akigeuka nyuma, nafsi yangu haifurahii kwake.”

04 Mwanzo 15:6

Abramu akamtumaini BWANA, na BWANA akalihesabu tumaini hilo kuwa haki kwake.

05 Warumi 3:28

Kwa maana tuna hakika kwamba mtu anahesabiwa haki kwa imani, bila matendo ya sheria.

06 Wafilipi 3:9

na nionekane kuwa ndani yake, bila haki yangu mwenyewe inayotokana na kuishika sheria, bali nikiwa na haki inayopatikana kupitia imani katika Kristo: haki itokayo kwa Mungu, inayotegemea imani.

Mada zinazohusiana