Mistari ya Biblia Kuhusu Thawabu

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Thawabu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Wakorintho 3:14

Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu yake.

02 Mathayo 6:20

Lakini jiwekeeni hazina mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba.

03 Wakolosai 3:23-24

Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia.

04 Waebrania 11:6

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.

05 Mathayo 16:27

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

06 Ufunuo 22:12

“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.

Mada zinazohusiana