Mistari ya Biblia Kuhusu Mbinguni
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Mbinguni ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Katika nyumba ya Baba yangu kuna makao mengi. La sivyo ningewaambia, kwa maana ninakwenda kuwaandalia mahali. Na nikiisha kwenda na kuwaandalia mahali, nitarudi na kuwachukua ili mkae pamoja nami, ili ninyi pia mwe pale nilipo.
Lakini uraia wetu uko mbinguni, na kutoka huko tunamsubiri kwa shauku Mwokozi, Bwana Yesu Kristo,
Mmefufuliwa pamoja na Kristo; kwa hiyo tafuteni yale yaliyo juu, mahali ambapo Kristo ameketi upande wa kulia wa Mungu. Elekezeni mawazo yenu kwenye mambo ya juu, wala si kwenye mambo ya duniani.
Kwa maana tunajua kwamba ikiwa hema tunamoishi hapa duniani itang’olewa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba ambayo haikujengwa kwa mikono ya wanadamu, ya milele, mbinguni.
Kila chozi atalifuta kutoka machoni mwao. Kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu. Mambo ya zamani yamepita.”
Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, kweli, na uzima. Mtu yeyote anakuja kwa Baba kupitia kwangu tu.
Lakini kwa hali ilivyo, wanajitahidi kuifikia nchi iliyo bora zaidi: nchi iliyo mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni kuwa ni aibu kujulikana kama Mungu wao, naye amewaandalia mji.
na katika urithi ambao hauwezi kamwe kuoza, wala kuchafuliwa, wala kunyauka. Urithi huo unahifadhiwa salama mbinguni kwa ajili yenu,
Badala yake, jilimbikizieni hazina mbinguni, ambako nondo wala kutu haziwezi kuziharibu, na hakuna wezi wa kutoboa kuta na kuziiba.
Lakini msifurahi kwa sababu roho hao wanawatii. Afadhali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”