Mistari ya Biblia Kuhusu Bwana, Tuongezee Imani
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Bwana, Tuongezee Imani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mitume walimwambia Bwana, “Tupe imani zaidi!”
Mara moja baba wa mtoto akapaza sauti, “Ninaamini! Nisaidie pale imani yangu inapopungua!”
Bwana alijibu, “Kama mngekuwa na imani yenye ukubwa wa mbegu ya haradali, mngeweza kuuambia mforsadi huu, ‘Jing’oe na mizizi yako, ukajipande baharini,’ nao ungefanya mnavyosema.
Aliwaambia, “Ni kwa sababu imani yenu ni ndogo mno. Kweli nawaambia, kama mna imani hata iliyo ndogo kama mbegu ya haradali, mnaweza kuuambia mlima huu, ‘Toka hapa uende pale,’ nao utakwenda. Hakuna jambo ambalo hamtaweza kulifanya.”
Tumkazie macho Yesu, kiongozi aliyetutangulia katika imani na anayeikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa mbele yake, alivumilia msalaba na kuihesabu aibu yake kuwa si kitu, kisha ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.
Yesu akamwambia, “’Kama unaweza!’ Kila kitu kinawezekana kwa mtu anayeamini.”
Kwa maana ni kwa neema hiyo mmeokolewa, kupitia imani. Jambo hili halitoki kwenu; ni zawadi ya Mungu.
Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu kwa ajili yenu nyakati zote, na ni haki tufanye hivyo, kwa sababu imani yenu inakua kupita kiasi, na upendo alio nao kila mmoja wenu kwa wengine unazidi kuongezeka.
Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isikome. Nawe, utakapokuwa umerudi, uwatie nguvu ndugu zako.”