Mistari ya Biblia Kuhusu Imani Hutokana na Kusikia

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Imani Hutokana na Kusikia ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Warumi 10:17

Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo.

02 Yohana 20:31

Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

03 Wagalatia 3:2

Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia?

04 1 Petro 1:23

Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele.

05 Warumi 10:14

Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria?

06 Warumi 10:8

Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, lile neno la imani tunalolihubiri.

07 Yohana 17:20

“Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao

08 Matendo 4:4

Lakini wengi waliosikia lile neno waliamini, idadi yao ilikuwa yapata wanaume 5,000.

Mada zinazohusiana

Kutoka kwa miongozo