Mistari ya Biblia Kuhusu Taji

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Taji ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 7 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 2 Timotheo 4:8 Mstari mkuu

Sasa ninangojewa na taji la haki, ambalo Bwana, hakimu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi tu, bali pia wote waliotamani kudhihirishwa kwake.

02 1 Petro 5:4

Kisha Mchungaji Mkuu atakapofunuliwa, mtapewa taji la utukufu ambalo halitanyauka kamwe.

03 Yakobo 1:12

Heri mtu anayestahimili wakati wa jaribu. Akishathibitishwa kuwa halisi, atapokea taji la uzima ambalo Mungu amewaahidi wale wanaompenda.

04 Ufunuo 2:10

Usiogope lolote kati ya mateso yatakayokupata. Tazama, Ibilisi anakaribia kuwatupa baadhi yenu gerezani, ili mjaribiwe, nanyi mtapata dhiki kwa siku kumi. Dumu katika uaminifu hata kufikia kifo, nami nitakupa taji la uzima.

05 1 Wakorintho 9:25

Kila mshindani hujinyima mambo mengi katika mazoezi yake. Wao hukubali hivyo ili washinde shada linalonyauka upesi; sisi, ili tushinde shada lisilonyauka kamwe.

06 Ufunuo 3:11

Ninakuja hivi karibuni. Kishike kwa nguvu kile ulicho nacho, ili mtu yeyote asije akalichukua taji lako.

Je, hamjui kwamba kila mkimbiaji uwanjani hushindana mbio, lakini ni mmoja tu anayepewa tuzo? Kimbieni kama yeye, ili mshinde tuzo. Kila mshindani hujinyima mambo mengi katika mazoezi yake. Wao hukubali hivyo ili washinde shada linalonyauka upesi; sisi, ili tushinde shada lisilonyauka kamwe.

Mada zinazohusiana