Mistari ya Biblia Kuhusu Mahali Palipotayarishwa
Mistari 13 ya Biblia kuhusu Mahali Palipotayarishwa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Na nikiisha kwenda na kuwaandalia mahali, nitarudi na kuwachukua ili mkae pamoja nami, ili ninyi pia mwe pale nilipo.
Katika nyumba ya Baba yangu kuna makao mengi. La sivyo ningewaambia, kwa maana ninakwenda kuwaandalia mahali.
Lakini kwa hali ilivyo, wanajitahidi kuifikia nchi iliyo bora zaidi: nchi iliyo mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni kuwa ni aibu kujulikana kama Mungu wao, naye amewaandalia mji.
Hakuna mji hapa unaotubakia; mji tunaoutazamia ni ule ambao bado unakuja.
Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi: “Tazama, makao ya Mungu yako pamoja na wanadamu! Atafanya makao yake pamoja nao, nao watakuwa jamii za watu wake; Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
“Mioyo yenu isifadhaike. Mwaminini Mungu, na niaminini mimi vilevile.
Kwa maana tunajua kwamba ikiwa hema tunamoishi hapa duniani itang’olewa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba ambayo haikujengwa kwa mikono ya wanadamu, ya milele, mbinguni.
Lakini uraia wetu uko mbinguni, na kutoka huko tunamsubiri kwa shauku Mwokozi, Bwana Yesu Kristo,
Nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kutoka kwa Mungu, ukiwa tayari kama bibi arusi aliyejipamba kwa ajili ya mume wake.
Yesu alimjibu, “Kweli nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami katika paradiso.”
Kwa maana alikuwa akiungojea mji wenye misingi imara, mji uliosanifiwa na kujengwa na Mungu.
na katika urithi ambao hauwezi kamwe kuoza, wala kuchafuliwa, wala kunyauka. Urithi huo unahifadhiwa salama mbinguni kwa ajili yenu,
Mmefufuliwa pamoja na Kristo; kwa hiyo tafuteni yale yaliyo juu, mahali ambapo Kristo ameketi upande wa kulia wa Mungu. Elekezeni mawazo yenu kwenye mambo ya juu, wala si kwenye mambo ya duniani.