Mistari ya Biblia Kuhusu Uthabiti
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Uthabiti ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Basi, ndugu zangu wapendwa, simameni imara bila kutikisika, mkizidi kufanya kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa mnajua kwamba katika Bwana kazi yenu ngumu haipotei bure.
kwa maana mnajua kwamba imani yenu inapopimwa, upimaji huo hutokeza ustahimilivu. Acheni ustahimilivu ukamilishe kazi yake, ili mkomae na kuwa kamili, bila kukosa chochote.
ikiwa tu mnadumu katika imani, mkiwa imara juu ya msingi wenu na thabiti, bila kuyumbishwa mbali na tumaini mlilopewa katika Injili mliyoisikia. Injili hii imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, nami Paulo nimekuwa mtumishi wake.
Nimemweka BWANA mbele yangu wakati wote; kwa kuwa yupo pale mkono wangu wa kuume, sitajikwaa kamwe.
Simameni imara dhidi yake, mkiishikilia imani yenu. Mnajua kwamba ndugu zenu kote ulimwenguni wanavumilia mateso hayo hayo.
Kaeni macho. Simameni imara katika imani. Kuweni jasiri na hodari.
Heri mtu anayestahimili wakati wa jaribu. Akishathibitishwa kuwa halisi, atapokea taji la uzima ambalo Mungu amewaahidi wale wanaompenda.
Tumaini hili ni letu kama nanga ya nafsi, nanga inayoshika salama na imara, nayo hufika katika sehemu ya ndani nyuma ya pazia.
Kwa hiyo, wapendwa, kwa kuwa mmeambiwa haya mapema, kaeni macho. Msikubali upotofu wa watu wasiofuata sheria uwachukue na kuwaangusha kutoka mahali penu imara.
Habari mbaya haziwatishi; mioyo yao iko imara kwa sababu wanamtumaini BWANA.
Sasa tunaweza kuishi kweli tena, ikiwa mnasimama imara katika Bwana.