Mistari ya Biblia Kuhusu Kumaliza Mbio

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Kumaliza Mbio ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 12 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 2 Timotheo 4:7 Mstari mkuu

Nimeshindana shindano zuri, nimemaliza mbio, nimeilinda imani.

02 Matendo 20:24

Lakini sioni maisha yangu kuwa na thamani yoyote, kana kwamba ni ya thamani kwangu. Ninachotaka tu ni kumaliza mbio zangu na kukamilisha huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu: kuishuhudia kikamilifu Injili ya neema ya Mungu.

03 1 Wakorintho 9:24

Je, hamjui kwamba kila mkimbiaji uwanjani hushindana mbio, lakini ni mmoja tu anayepewa tuzo? Kimbieni kama yeye, ili mshinde tuzo.

04 Wafilipi 3:14

nami ninakimbia moja kwa moja kuelekea lengo ili nishinde tuzo iliyoahidiwa na mwito wa Mungu wa kwenda juu katika Kristo Yesu.

05 Waebrania 12:1-2

Basi, kwa kuwa nasi tumezungukwa pande zote na wingu la mashahidi lililo kubwa hivyo, tuvue kila mzigo, pamoja na dhambi inayojifunga kwetu kwa urahisi, tukimbie mbio zilizopangwa mbele yetu, na tuzikimbie kwa saburi. Tumkazie macho Yesu, kiongozi aliyetutangulia katika imani na anayeikamilisha. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa mbele yake, alivumilia msalaba na kuihesabu aibu yake kuwa si kitu, kisha ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

06 Yohana 17:4

Nimekutukuza duniani kwa kuikamilisha kazi uliyonipa niifanye.

07 Yohana 19:30

Yesu alipokwisha kuipokea divai chungu, alisema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.

08 2 Timotheo 4:8

Sasa ninangojewa na taji la haki, ambalo Bwana, hakimu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi tu, bali pia wote waliotamani kudhihirishwa kwake.

09 1 Wakorintho 9:25

Kila mshindani hujinyima mambo mengi katika mazoezi yake. Wao hukubali hivyo ili washinde shada linalonyauka upesi; sisi, ili tushinde shada lisilonyauka kamwe.

10 Ufunuo 2:10

Usiogope lolote kati ya mateso yatakayokupata. Tazama, Ibilisi anakaribia kuwatupa baadhi yenu gerezani, ili mjaribiwe, nanyi mtapata dhiki kwa siku kumi. Dumu katika uaminifu hata kufikia kifo, nami nitakupa taji la uzima.

11 Luka 9:62

Yesu akajibu, “Hakuna mtu anayeshika plau kwa mkono kisha akaendelea kutazama nyuma anayefaa kwa ufalme wa Mungu.”

12 Waebrania 12:1

Basi, kwa kuwa nasi tumezungukwa pande zote na wingu la mashahidi lililo kubwa hivyo, tuvue kila mzigo, pamoja na dhambi inayojifunga kwetu kwa urahisi, tukimbie mbio zilizopangwa mbele yetu, na tuzikimbie kwa saburi.

Mada zinazohusiana