Mistari ya Biblia Kuhusu Si Mwepesi wa Hasira

Mistari 5 ya Biblia kuhusu Si Mwepesi wa Hasira ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 103:8

Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

02 Kutoka 34:6

Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “ Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu,

03 Hesabu 14:18

‘ Bwana si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’

04 Zaburi 86:15

Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.

05 Yoeli 2:13

Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni Bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.

Mada zinazohusiana