Mistari ya Biblia Kuhusu Nuru ya Ulimwengu
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Nuru ya Ulimwengu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa juu ya kilima hauwezi kufichika.
Vilevile, nuru yenu inapaswa kung’aa mahali ambapo watu wanaweza kuiona, ili waone matendo yenu mazuri na kumtukuza Baba yenu wa mbinguni.
Hapo zamani ninyi mlikuwa giza lenyewe; sasa, katika Bwana, ninyi ni nuru. Kwa hiyo ishini kama watoto wa nuru.
ili mtu yeyote asiweze kuwalaumu, nanyi mbaki safi, watoto wa Mungu wasio na dosari katikati ya kizazi kilichopotoka na kuharibika. Kati ya watu hao mnang’aa kama nyota ulimwenguni
Yesu akasema nao tena: “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Wale wanaonifuata hawatatembea gizani kamwe; watakuwa na nuru ya uzima.”
Msishiriki matendo ya giza, ambayo hayazai kitu chochote chema. Badala yake yaonyesheni wazi jinsi yalivyo.
Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si watu wa usiku wala wa giza.
Kwa maana hii ndiyo amri ambayo Bwana ametupa: ‘Nimekuweka kuwa nuru kwa mataifa, ili uwe njia ya wokovu mpaka sehemu za mbali kabisa za dunia.’”
Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru, ili mpate kuwa wana wa nuru.” Yesu alipokwisha kusema hayo, aliondoka akajificha mbali nao.
Usiku unakaribia kwisha; mchana u karibu. Kwa hiyo tuvue kama nguo matendo yaliyo ya giza, na tuvae deraya ya nuru.
Lakini tukitembea katika nuru, kama vile yeye alivyo katika nuru, tuna ushirika sisi kwa sisi, na damu ya Yesu, Mwana wake, inaendelea kutusafisha kutoka kila dhambi.
Kwa maana Mungu aliyesema, “Kutoka gizani nuru itaangaza,” ndiye aliyeangaza mioyoni mwetu, ili kuleta nuru ya kuujua utukufu wa Mungu, utukufu unaoonekana katika uso wa Kristo.