Yeremia 45

Neno: Kiswahili Contemporary Version

1Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule:

2“Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku:

3Ulisema, ‘Ole wangu! Bwana ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

4Bwana akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kungʼoa kile nilichokipanda katika nchi yote.

5Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asema Bwana, lakini popote utakapokwenda, nitayaokoa maisha yako.’ ”

Yeremia

Open the interactive reader to switch translations, adjust type, and mark verses — or browse verses by topic.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License