Mistari ya Biblia Kuhusu Kumfuata Yesu

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Kumfuata Yesu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 8 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Luka 9:23 Mstari mkuu

Kisha akawaambia wote, “Yeyote anayetaka kuja nyuma yangu ni lazima ajikane, aubebe msalaba wake kila siku, na aendelee kunifuata.

02 Yohana 10:27

Kondoo walio wangu huisikiliza sauti yangu; nawajua, nao hunifuata.

03 Mathayo 4:19

Aliwaambia, “Njooni, mnifuate, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.”

04 Yohana 12:26

Yeyote anayenitumikia lazima anifuate, na mtumishi wangu atakuwa pale nilipo. Baba atamheshimu yeyote anayenitumikia.

05 Marko 8:34

Kisha akauita umati pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Mtu yeyote anayetaka kuja nyuma yangu ni lazima ajikatae mwenyewe, abebe msalaba wake, na anifuate.

06 Yohana 8:12

Yesu akasema nao tena: “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Wale wanaonifuata hawatatembea gizani kamwe; watakuwa na nuru ya uzima.”

07 1 Petro 2:21

Ni kwa ajili ya hili Mungu aliwaita, kwa sababu Kristo pia aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia mfano wa kunakili, ili mtembee katika nyayo zake.

08 Mathayo 16:24

Kisha Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Yeyote anayetaka kuja nyuma yangu lazima ajikane, aubebe msalaba wake, na anifuate.

Mada zinazohusiana