Nehemia 7

Neno: Kiswahili Contemporary Version

1Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa.

2Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine.

3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

4Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu.

5Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

6Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,

7wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana): Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:

8wazao wa Paroshi 2,172

9wazao wa Shefatia 372

10wazao wa Ara 652

11wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818

12wazao wa Elamu 1,254

13wazao wa Zatu 845

14wazao wa Zakai 760

15wazao wa Binui 648

16wazao wa Bebai 628

17wazao wa Azgadi 2,322

18wazao wa Adonikamu 667

19wazao wa Bigwai 2,067

20wazao wa Adini 655

21wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98

22wazao wa Hashumu 328

23wazao wa Besai 324

24wazao wa Harifu 112

25wazao wa Gibeoni 95

26watu wa Bethlehemu na Netofa 188

27watu wa Anathothi 128

28watu wa Beth-Azmawethi 42

29watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743

30watu wa Rama na Geba 621

31watu wa Mikmashi 122

32watu wa Betheli na Ai 123

33watu wa Nebo 52

34wazao wa Elamu 1,254

35wazao wa Harimu 320

36wazao wa Yeriko 345

37wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721

38wazao wa Senaa 3,930

39Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973

40wazao wa Imeri 1,052

41wazao wa Pashuri 1,247

42wazao wa Harimu 1,017

43Walawi: wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74

44Waimbaji: wazao wa Asafu 148

45Mabawabu wa malango: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138

46Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,

47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,

48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,

49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,

50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,

51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,

52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,

53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,

54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,

55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,

56wazao wa Nesia na Hatifa.

57Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,

58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,

59wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.

60Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392

61Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:

62wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642

63Na kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).

64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.

65Kwa hiyo, mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.

66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;

67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245.

68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245

69ngamia 435 na punda 6,720.

70Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.

71Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu, na mane 2,200 za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

72Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

73Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe. Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Nehemia

Open the interactive reader to switch translations, adjust type, and mark verses — or browse verses by topic.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License